Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Mohammad Baqir Qalibaf, Spika wa Bunge la Kiislamu la Iran, aliandika kwenye ukurasa wake binafsi katika mitandao ya kijamii baada ya kukutana na Sardar Ayaz Sadiq, Spika wa Bunge la Kitaifa la Pakistan, akisema: “Leo nimeelekea nchini Pakistan kwa mwaliko maalumu wa Mheshimiwa Sardar Ayaz Sadiq, Spika wa Bunge la Kitaifa la Pakistan. Kuimarisha uhusiano wa pande mbili kati ya mataifa haya mawili ndugu - hasa katika nyanja za ushirikiano wa kiuchumi na kiusalama - ndilo lengo kuu la safari hii.”
Akiendelea kueleza, Qalibaf alisema kuwa katika mazungumzo yake na Bw. Sadiq, alishukuru Pakistan kwa uungaji mkono wake usio na kikomo wakati wa uvamizi wa utawala wa Kizayuni, na akaielezea Pakistan kuwa “rafiki wa kweli katika nyakati zote.” Pia walijadili masuala kadhaa yanayohusu kuimarisha ushirikiano wa pamoja.
Kwa upande wake, Spika wa Bunge la Kitaifa la Pakistan alisisitiza kuwa Iran ni jirani na ndugu wa kuaminika kwa Pakistan, na akabainisha kuwa bunge na serikali ya nchi hiyo daima wamesimama bega kwa bega na Iran.
Aidha, alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa serikali na wananchi wa Iran kwa ushindi dhidi ya utawala wa Kizayuni katika vita vya siku 12.
Your Comment